Home Sports SIMBA NA YANGA ZASHINDANA KUCHANGA MKWANJA

SIMBA NA YANGA ZASHINDANA KUCHANGA MKWANJA

WATANI wa jadi Yanga na Simba kupitia Azam TV wamefungua kampeni ya NANI ZAIDI ambayo itakuwa inawahusisha mashababiki wa timu hizo mbili ambao watakuwa wanashindana kuchangia pesa kwenye timu zao.

Watachangia pesa hizo kupitia mitandao ya simu ikiwa ni Tigo, Airtel na Vodacom kisha baadaye mshindi atachaguliwa na kutangazwa.

Mtendaji Mkuu wa Simba,(CEO), Barbra Gonzalez amesema kuwa anaomba mashabiki wa Simba waweze kuchanga pesa kwa wingi kwa ajili ya timu yao.

“Michango hiyo itatumika katika ujenzi wa uwanja.Mimi nilienda Doha,Qatar na Mwenyekiti wetu alienda Uturuki kuangalia viwanja, hivyo Wanasimba wanatakiwa kuchangia,”.

Kwa upande wa Yanga ni CEO, Senzo Mbatha amesema kuwa Yanga wanatakiwa kuchangia pesa nyingi ili waweze kuongoza kama ambavyo wanaongoza kwenye ligi.

“Wakati nakuja Tanzania nilipoona mashabiki wanapenda mpira niliona pesa kubwa sana, shida kubwa ilikuwa katika kuipata kupitia mradi huu naomba kwa mashabiki wa Yanga waongoze kuchangia,” amesema.

Kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi Juni 2,2022 na viongozi mbalimbali walikuwepo pamoja na waandishi.

Previous articleMSHINDI WA MILIONI 20 NA MERIDIANBET ANENA MBINU YA USHINDI!
Next articleSTARS YAWASILI BENINI,YABEBA MATUMAINI