WAYDAD WATWAA TAJI LA TATU LIGI YA MABINGWA AFRIKA

MABINGWA wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni Wydad baada ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mohamed V.

Linakuwa ni taji la tatu kwa timu hiyo ya Morroco kuweza kutwaa baada ya kuanza kufanya hivyo 1992 na 2017.

Zouhair El Moutaraji aliweza kuwa shujaa kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa mbele ya Al Ahly kwa kufunga mabao yote mawili yaliyoipa taji timu ya Wydad Casabalanca kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Alipachika mabao hayo ilikuwa ni dakika ya 15 na lile la pili ilikuwa ni dakika ya 48 hivyo waliugawa mchezo katika dakika 15 za mwanzo kipindi cha kwanza na dakika 15 za pili za kipindi cha pili.

Rammy Rabia aliweza kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo na kuwafanya Al Ahly kukamilisha mchezo wakiwa pungufu kwa kuwa ilikuwa ni dakika ya 90+2 za mchezo huo.

Ni mashuti 14 Al Ahly ya Misri walipiga huku mawili pekee yakilenga lango na Wydad walipiga jumla ya mashuti 11 na ni matatu yalilenga lango katika mchezo huo.