IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ipo kwenye hesabu za kuwania saini ya Mustafa Kiza.
Nyota huyu ni beki raia wa Ugada hivyo anakuja kuongeza nguvu kwenye upande wa ulinzi ndani ya kikosi hicho.
Yanga imekuwa imara kwenye upande wa mabeki msimu huu ikiwa ni timu namba moja iliyofungwa mabao machache kwenye ligi ambayo ni 7 baada ya kucheza mechi 26.
Inaongoza ligi ikiwa na pointi 64 kibindoni kwa msimu wa 2021/22.