MASTAA WATATU SIMBA WAWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA

 WACHEZAJI watatu wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco wanawania tuzo ya mchezaji bora.

Tuzo hiyo ni maalumu kwa ajili ya mashabiki ambao wamekuwa wakichagua mchezaji kupitia njia ya mtandao kwa kumpigia kura mchezaji wanayempenda ili aweze kusepa na tuzo hiyo.

Ni kiungo mzawa Mzamiru Yassin kiungo wa kazi, Rally Bwalya pia ambaye ni kiungo yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo.

Kibu Dennis ni mshambuliaji pekee ambaye yupo kwenye orodha ya wachezaji ambao wanawania tuzo hiyo.