MSHINDI WA BILIONI ZA JACPOT YA SPORTPESA AWEKA WAZI MIPANGO YAKE

KIJANA Florian Valerian Massawe mshindi wa JACKPOT ya SportPesa ya shilingi 1,255,316,060 (bilioni 1.25) leo Mei 25 ameweka wazi mipango yake.

Katika mahojiano maalum na Global Radio kwenye kipindi cha Krosi Dongo, Massawe amesema mpango wake mkubwa kwa sasa ni kuweza kuwekeza kwenye masuala ya Garage kwa kuwa yeye ni fundi na hana mpango wa kuiacha hiyo kazi.

“Nina mpango wa kuweza kufungua Garage kubwa ya kisasa ambayo itakuwa itakuwa na kila kitu kwa kuwa kwa sasa nimeajiriwa kwenye kampuni na bado ninafanya hiyo kazi.

“Sina mpango wa kuweza kuiacha kazi yangu hii,nimesomea na ninaendelea kuifanya hasa ukizingatia kwamba kuna watu ambao wamekuwa wakinipigia simu kuweza kujua kuhusu masuala yangu ya ufundi na ninawaelekeza,” amesema.