Home Sports KILA KITU KIWE KWA MIPANGO LALA SALAMA KWENYE LIGI

KILA KITU KIWE KWA MIPANGO LALA SALAMA KWENYE LIGI

KWA sasa kila mtu anaona namna ligi ilivyo huku kila mmoja akipambana kutimiza malengo yake binafsi pamoja na ya timu ambayo haya ni muhimu kuweza kupatikana kisha mchezaji itakuwa ni baadaye katika kufanya majukumu yake.

Pongezi kubwa kwa makocha kwa msimu huu wameweza kwenda na ile kasi ambayo walianza nayo tangu mwanzo wa msimu mpaka mwisho wa msimu unaokaribia kufika kwa sasa.

Kila mmoja anafanya kazi na kazi inaonekana kupitia matokeo ambayo yanapatikana uwanjani hili jambo kubwa linastahili pongezi.

Mwendo mzuri na kila mmoja anasaka ushindi kila anapopata nafasi hii inapendeza kuona kazi nzuri zinafanywa iwe ni kwa makocha wazawa hata wale wa kigeni nao wamekuwa wakifanya kweli.

Mzunguko wa kwanza niliweka wazi kwamba hakuna kulemaa na kutegemea kuzinduka mwisho ukiaanza kwa kasi nenda nayo mpaka mwisho ili upate unachostahili.

Imekuwa hivyo tangu mchezo wa kwanza na sasa ni muda wa ngwe ya pili wachezaji wanafanya kweli na makocha wanakuja na mbinu tofauti.

Matatizo yapo hasa kwenye sehemu za kuchezea ambalo limekuwa ni tatizo kwa kila timu zile ambazo zina viwanja ambavyo havina ubora.

Tumeona kwamba kuna wakati viwanja vilifungiwa kupisha maboresho na yote hii ilitokana na kutokidhi ule ubora ambao unahitajika.

Hapa kwa hili ni wamiliki wa timu wenyewe wana uwezo wa kulitatua hili kwa kuongeza uwekezaji katika umiliki wa viwanja vyao binafsi.

Kama ilivyo kwa Azam FC wao wameweza kufanya kweli kwenye uwekezaji huu ni mfano wa kuigwa na wana viwanja viwili vya kufanyia mazoezi ikiwa ni kile cha nyasi bandia na nyasi asilia ni kitu kizuri.

Pia mazingira ya wachezaji wanaoishi Azam FC ni katika hali ya utulivu kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa kupenda na kufurahi kwa sababu kila kitu kipo.

Hapa sasa kwa timu ambazo zina mpango wa kuweza kumiliki viwanja vyao nina amini kwamba wanaweza kupata somo la bure kwa Azam ambao hawana tatizo na mtu.

Jambo lingine ni kuhusu wachezaji wenyewe kuweza kutulia kwa wakati huu wa lala salama kwa kuwa wengi wamekuwa na presha kubwa wawapo uwanjani.

Suala la presha wakati mwingine limewafanya wakafanya makosa kwa kuwaumiza wengine hili sio sawa ni lazima watulie na wafanye kazi kwa umakini katika kutimiza majukumu yao.

Kila la kheri kwa timu kwa mechi ambazo zimebaki kwa zilizopanda daraja zinajua kwamba ugumu wa Championship ulivyo na namna ambavyo walipambana kufika hapa hivyo hawatapuuzia.

DTB na Ihefu ni timu ambazo zinatambua kuhusu hali ilivyokuwa mpaka kufika hapa ikiwa zitafeli kwa wakati ujao basi itakuwa ni nafasi yao nyingine kuweza kurudia ule ushindani wa Championship.

Previous article8 BORA LIGI YA SOKA LA UFUKWENI KUANZA
Next articleMSHINDI WA BILIONI ZA JACPOT YA SPORTPESA AWEKA WAZI MIPANGO YAKE