PRINCE DUBE KUIKOSA RUVU SHOOTING

 MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Prince Dube anatarajiwa kuukosa mchezo wa leo kati ya Ruvu Shooting v Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mabatini,Pwani.

Dube ambaye msimu uliopita wa 2020/21 alikuwa kwenye ubora mkubwa aliweza kutupia mabao 14 msimu huu ameweza kutupia bao moja na pasi moja ya bao.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Azam FC, Ahamid Moallin amesema kuwa kuna wachezaji ambao wanaweza kuukosa mchezo wa leo kutokana na kutokuwa fiti.

“Prince Dube anaweza kukosekana kwenye mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting lakini asilimia kubwa tutasubiri ripoti ya madaktari.

“Pia kipa  Salula, (Ahmed) naye pia kuna hatihati anaweza kuukosa mchezo huo ila wachezaji wengine wapo tayari kuweza kupambana na kupata pointi tatu muhimu,” amesema.

Azam FC imetoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wao uliopita wa ligi, wanakwenda kukutana na Ruvu Shooting ambayo metoka kugawana pointi mojamoja na Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.