Home International KOCHA ARSENAL ANA MAUMIVU KWELI

KOCHA ARSENAL ANA MAUMIVU KWELI

MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa bado wana maumivu ndani yake kwa kuwa walifanya makosa mbele ya Newcastel United ndiyo maana licha ya ushindi mbele ya Everton haukuweza kuwasaidia.

Arsenal imemaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kama wangeweza kuchanga karata yao vema wangemaliza nafasi ya nne na kupata fursa ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ni pointi 69 wamemaliza nazo msimu huu na watashiriki michuano ya Europa League baada ya kuichapa mabao 5-0 Newcastel United kwenye mchezo wa mwisho.

“Kupata nafasi ya kucheza UEFA ilikuwa ni miujiza kama ingetokea katika mechi yetu ya mwisho japo tulishinda lakini haikuweza kutusaidia chochote na ukweli ni kwamba bado nina maumivu,”.

Previous articleUTAZAME UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA
Next articleAZAM FC WANASUBIRI TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI