NENO LA GUARDIOLA BAADA YA UBINGWA WA LIGI KUU ENGLAND

KOCHA Mkuu wa Manchester City ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England amesema kuwa ilikuwa ni pointi nyingi wapinzani wao wamemaliza nazo msimu huu.

Ilikuwa ni Liverpool ambao walikuwa wanavutana na Manchester City na tofauti yao ni pointi moja pekee.

City imeshinda mchezo wake dhidi ya Aston Villa kwa mabao 3-2 ikiwa Uwanja wa Etihad na ilifanya kazi kubwa ya kupindua meza kwa kuwa walitanguliwa na wapinzani wao.

Pep amesema:”92 ni pointi nyingi sana na ambazo zinashangaza kwa wapinzani wetu ila ni wakati wetu wa kuweza kuona kwamba wakati ujao tunakuwa imara.

“Kupata kwetu ubingwa ni furaha na kila mmoja ameweza kupata kile ambacho tulikuwa tunastahili hivyo ni furaha kwa kila ambaye alikuwa nasi,”.

IIkay Gundogan alipachika mabao mawili ilikuwa dk ya 76 na 81 na bao moja lilipachikwa na Rodri dk ya 78.

Yale ya Aston Villa ambao walianza kufunga yalipachikwa na Matty Cash dk ya 37 na msumari wa pili uligota kwa Phillippe Countinho ilikuwa dk ya 69.