MANCHESTER CITY MABINGWA LIGI KUU ENGLAND

MANCHESTER City wameweza kutetea taji lao la Ligi Kuu England baada ya kuweza kupindua meza mbele ya Aston Villa. Katika dakika 45 za mwanzo Aston Villa walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0 lakini kipindi cha pili waliweza kushuhudia wakifungwa mabao 3-2 na kuifanya City kufikisha pointi 93 ndani ya Ligi Kuu England. Liverpool wao wameshinda mabao…

Read More

GEITA GOLD YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA SIMBA

DAKIKA 90 zimekamilika Uwanja wa CCM Kirumba kwa timu zote kugawana pointi mojamoja za ligi. Ni bao la George Mpole dk ya 20 na Kibu Dennis dk ya 27 kwa pasi ya Rally Bwalya kwenye mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wazi kwamba kila timu ilikuwa na nafasi ya kushinda. Sasa Mpole anafikisha mabao 14…

Read More

CCM KIRUMBA:GEITA GOLD 1-1 SIMBA

 KABLA ya mchezo kuanza Uwanja wa CCM Kirumba, George Mpole mshambuliaji wa Geita Gold na Kocha Mkuu, Felix Minziro wamekabidhiwa tuzo zao za mwezi Aprili. Minziro alichaguliwa kuwa kocha bora na Mpole mwenye maao 14 akiwa ni mchezaji bora wa mwezi uliopita. Ubao kwa sasa unasoma Geita Gold 1- Simba ikiwa ni mapumziko kwenye mchezo…

Read More

MANULA NJE,BENO,LWANGA,GADIEL NDANI

IKIWA ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold, Simba inatarajia kushuka na kikosi kazi huku kipa namba moja Aishi Manula leo akiwa nje. Kikosi kipo namna hii:- Beno Kakolanya Shomari Kapombe Gadiel Michael Joash Onyango Pascal Wawa Kibu Dennis Kanoute Sadio John Bocco Rally Bwalya Pape Sakho Taddeo Lwanga

Read More

SIMBA YAHOFIA MECHI YAO DHIDI YA GEITA GOLD

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mchezo wao wa leo dhidi ya Geita Gold utakuwa mgumu kutokana na aina ya wapinzani ambao wanakutana nao. Simba wenye pointi 50 kibindoni wana kibarua cha kusaka pointi tatu nyingine leo mbele ya Geita Gold saa 10:00 jioni Uwanja wa CCM Kirumba huku Geita Gold nao wakiwa…

Read More

RUVU SHOOTING WAANZA SAFARI KUREJEA PWANI

MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar umeshamalika hivyo wameanza safari ya kurejea Dar. Jana Ruvu Shooting ilitoshana nguvu bila kufungana na Kagera Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-0 Ruvu Shooting na kuwafanya wagawane pointi mojamoja…

Read More

MZAMBIA SIMBA APEWA MKATABA WA KAZI KISA LWANGA

IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco amelazimika kumuongezea kandarasi kiungo wa Zambia, Rally Bwalya kwa ajili ya msimu ujao. Sababu kubwa inatajwa kuwa ni kutokuwa fiti kwa kiungo mkata umeme Taddeo Lwanga raia wa Uganda. Kiungo Bwalya alisajiliwa Simba Agosti 15, 2020 akitokea Power Dynamos FC ya kwao Zambia alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada…

Read More