BOSI mpya wa Manchester United, Erik ten Hag amevunja mkataba wake ili kuiwahi klabu yake hiyo mpya tayari kwa kuweka mambo sawa.
Ten Hag alitarajiwa kumaliza mkataba wake na Ajax, Juni 30, mwaka huu, lakini Jumatatu alitarajiwa kutua ndani ya Manchester United lakini sasa ameondoka zikiwa zimesalia wiki sita kabla ya kumalizana na timu yake ya zamani.
Kocha huyo alitarajiwa kuanza kazi ndani ya Man United, Julai Mosi, mwaka huu, baada ya kusaini mkataba wake mpya na klabu hiyo.
Imeelezwa kuwa kocha huyo ameamua kwenda mapema ndani ya Man United kutokana na kuwa na mambo mengi ambayo anataka kuanza kuyaweka sawa.
Ten Hag amenukuliwa akisema: “Kuna mambo mengi ya kufanya (Man United) kama meneja lazima natakiwa kuanza kuweka vitu sasa hasa ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu ujao kuna mengi ya kufanya.
“Kama kwa upande wa stafu kuna mambo yanatakiwa kuweka sawa na kwa timu yaani wachezaji na masuala mengine mengi ndiyo maana natakiwa kuwa pale mapema zaidi.”
Kumbuka Ten Hag anaingia katika mtihani wa kuiongoza Man United msimu ujao baada ya kutoka kwenye msimu mbovu kuwahi kutokea ndani ya Premier League kwa misimu ya karibuni na ikiwa haijatwaa mataji yoyote kwa zaidi ya misimu mitano sasa.