MAYELE:MABEKI WANATAKA NISIFUNGE

FISTON Mayele,mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa mabeki wengi kwa sasa wamekuwa wakimkamia ili asifunge kila anapocheza.

Mayele msimu huu wa 2021/22 akiwa ndani ya kikosi cha Yanga amehusika kwenye mabao 15 kati ya 38.

Ametupia mabao 12 na kutoa pasi mbili za mabao hajafunga kwenye mechi nne za ligi msimu huu na kumfanya awe sawa mabao na mzawa George Mpole.

Mpole wa Geita Gold yeye ametupia mabao 12 na pasi 3 ndani ya kikosi cha Geita Gold.

Mayele amesema:”Wamekuwa wakipamana kwa kadri wanavyoweza ili kunizuia kufunga hilo ninajua na linanipa nguvu ya kupambana kwa ajili ya mechi zijazo.

“Ninajua kwamba ushindani ni mkubwa nami nitazidi kupambana ili kufikia malengo yangu na yale ya timu ambayo ni muhimu zaidi,” amesema