SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU MORRISON

UONGOZI wa Simba umesema kuwa ikiwa watapata taarifa kwamba mchezaji wao Bernard Morrison anahitajika na Yanga watawapa hata kwa mkopo.

Nyota huyo ambaye kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa muda kwa kile ambacho Kocha Mkuu, Pablo Franco wa Simba amesema kwamba ana majeraha amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilikuwa ni timu ya mwanzo Bongo kumtambulisha Morrison na mchezo wake wa kwanza alicheza ilikuwa dhidi ya Singida United zama za Luc Eymael.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa ikiwa Yanga wanamhitaji mchezaji huyo watapewa.

“Wanasema kwamba Yanga wanamhitaji Morrison ili aweze kuwafikisha hatua ya robo fainali? Sisi tutawapa mchezaji huyo hata kwa mkopo.

“Hatuna tatizo kwa sababu tunajua kwamba ikiwa hata wakibadili jina bado mambo yatabaki kuwa vilevile,”.