Home Sports TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI: POGBA, RONALDO, CONTE, MBAPPE, ERIKSEN, CARVALHO,...

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI: POGBA, RONALDO, CONTE, MBAPPE, ERIKSEN, CARVALHO, HAALAND

Manchester City wana nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 29, kwa uhamisho huru. (Mail)

Pogba angependa kufanya kazi na meneja Pep Guardiola na City wako tayari kumpatia ofa mshindi huyo wa Kombe la Dunia mkataba wa miaka minne. (Guardian)

Antonio Conte

Meneja wa Brighton Graham Potter ndiye anayependelewa kuchukua nafasi ya Antonio Conte katika Tottenham. Brighton wangetaka fidia ya pauni milioni 10 kutoka kwa Spurs iwapo Conte ataondoka mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

Conte ameitahadharisha Spurs kwamba watahitaji kugarimia sana kipindi hiki cha msimu huu la sivyo watakuwa na hatari ya kuhitaji “muujiza” kuzifikia timu nyingine. (Evening Standard)

Mshambuliaji Mreno Cristiano Ronaldo

Meneja ajaye wa Manchester United Erik ten Hag anamtaka mshambuliaji Mreno Cristiano Ronaldo kubakia katika klabu hiyo . Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake katika Old Trafford. (Telegraph)

Chelsea wanaangalia uwezekano wa uhamisho kwa ajili ya mlinzi Mbrazili Gleison Bremer, 25. (Football London)

Mshambuliaji Mfaransa wa klabu ya Reims Hugo Ekitike

Manchester United pia wana nia ya kumchukua mshambuliaji Mfaransa wa klabu ya Reims Hugo Ekitike mwenye umri wa miaka 19. (Mail)

Meneja wa Fulham Marco Silva anasema mshambuliaji Mreno Fabio Carvalho hatakuwa mchezaji ampya atakayepandishwa daraja msimu ujao. Liverpool wamekubali mkataba wenye thamani ya pauni milionii 7 £kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Liverpool Echo)

Christian Eriksen

Christian Eriksen anaangalia uwezekano wa kubakia katika Brentford msimu jao . Kiungo huyo wa kati wa Mdenmark mwenye umri wa miaka 30, amekuwa akihusishwa na taarifa za kurejea tena katika Tottenham na kuhamia Leicester. (Telegraph)

Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Juventus Mbrazili Arthur Melo, 25. (Ekrem Konur)

Mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappe

Mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappe, 23, atatangaza uamuzi wake wa mwisho juu ya iwapo ataondoka Paris St-Germain mwezi Juni au la. (Le Parisien – in French)

West Ham wanaangalia uwezekano wa kumhamisha kiungo wa katii wa Bunley mwenye umri wa miaka 26 Brownhill. (90Min)
mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland

Chanzo cha picha, Reuters

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland

Chelsea wamesikitika kuwa hawakuweza kusaini mkataba na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland, 21. Klabu hiyo iliwekewa ukomo katika uhamisho wa wachezaji kwasababu ya vikwazo dhidi ya Roman Abramovich kuhuatia uvamizi wa Urusi katika Ukraine. (ESPN)

The Hammers pia wanapanga dau kwa ajii ya mshambuliaji wa Chelsea Armando Broja baada ya kijana huyo mwenye numri wa miaka 20 kucheza vyema wakati akiwa katika mkataba wa mkopo katika Southampton. (Sun)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel nanasema mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku anaendelea kuwa sehemu muhimu ya mipango yake kwa ajili ya msimu ujao, licha ya mchezaji huyo mwenyeb umri wa miaka 28 kuhusishwa na taarifa za kurejea tena katika Inter Milan. (Mirror)

Meneja wa Leicester Brendan Rodgers ameazimia kukibadilisha kikosi chake katika hatua inayoweza kupelekea wachezaji kadhaa wa timu kuondoka katika klabu hiyo. (Mail)
Gavi

RAPHINHA

BARCELONA imepeleka ofa kwa Leeds United ikimtaka winga Mbrazili, Raphinha, 25. Leeds inapambana isishuke daraja Premier. (Telegraph)

LINGARD

KIUNGO Muingereza, Jesse Lingard, 29, anazivutia klabu za Juventus, Paris Saint-Germain, AC Milan na Newcastle wakati huu anapojiandaa kuondoka Manchester United baada ya kuitumikia kwa miaka 22. (Mail)

ZAHA

WINGA wa Crystal Palace na Ivory Coast, Wilfried Zaha, 29, haonekani kama atasaidia dili jipya klabuni hapo na anaweza kuuzwa katika kipindi kijacho cha usajili kwa kuwa mkataba wake unafikia tamati mwaka 2023. (Times)

TRAORE

BARCELONA haina mpango wa kulipa pauni milioni 25.3 ili kubadilisha dili la mkopo la winga wa Wolves, Adama Traore liwe la moja kwa moja, na watavutiwa tu na suala la kubadilishana wachezaji. (Fabrizio Romano)

LAUTARO

ARSENAL wanavutiwa kumsajili straika wa Inter Milan na Argentina, Lautaro Martinez, ingawa wakala wa nyota huyo mwenye miaka 24, hadhani kama ataondoka katika klabu yake ya sasa. (Goal)

Previous articleSALAH AWAONYA REAL MADRID, ATAKA KULIPIZA KISASI FAINALI UEFA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI