MADRID YASHINDA KIMAAJABU LIGI YA MABINGWA ULAYA

KLABU ya Real Madrid imeonyesha uimara wake kwa kupata ushindi wa maajabu katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kupindua matokeo mbele ya Manchester City.

Sasa Real Madrid inakwenda kukutana na Liverpool kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Liverpool huku Karim Benzema akifunga penalti ya ushindi kwa Real Madrid dk 95.

Real Madrid inafika hatua ya fainali ikiwa na jumla ya mabao 6-5 City.

Ilikuwa ni Uwanja wa Bernabeu walianza kwa kuzidiwa kwa kuwa Riyad Mahrez aliipa bao City dk ya 73 na kufanya iwe 5-3.

Mabao ya Real Madrid mengine yalifungwa na Rodrygo ambaye alikuwa benchi na alitupia mabao mawili ilikuwa dk ya 90 na 90+1.

Ngoma ni fainali nchini Ufaransa Mei 28 ili kupata bingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.