MANCHESTER City wakiwa na jambo lao hawazuilika baada ya wenyeji Leeds United kuchapwa mabao 4-0.
Wakiwa Uwanja wa Elland Road mbele ya mashabiki 35,771 kichapo hicho hakikuepukika kwenye michezo wa Ligi Kuu England.
Mabao ya Rodri dk 13,Nathan Ake dk ya 54, Gabriel Jesus dk 78 na Fernandinho dk ya 90+3 yalitosha kuwarejesha kileleni kwa mara nyingine tena kwa kuwa walishushwa kwa muda na Liverpool ambao waliichapa bao 1-0 Newcastle United.
Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa walipata tabu kupata ushindi huo ugenini.
Mchezaji bora wa mchezo huo uliokuwa na purukushani nyingi ni Phil Foden wa City.
Sasa City inafikisha pointi 83 ikiwa nafasi ya kwanza inafuatiwa na Liverpool nafasi ya pili yenye pointi 82 wakiwa tofauti ya pointi moja.