MAPILATO WA YANGA V SIMBA,PENALTI,KADI KAMA ZOTE

    MAPILATO wa mchezo wa leo wa Yanga v Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa unaambiwa weka mbali na watoto kutokana na rekodi zao kuwa ni za moto kila wanapochezesha mechi.

    Waamuzi ambao wapo kwenye orodha iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania ambao ni Ellyi Sasii, Mohamed Mkono, Frank Komba na Ramadhan Kayoko ambaye atakuwa mwamuzi wa kati hawa ni mapilato wa leo rekodi zao ni noma.

    Rekodi zinaonyesha kuwa Ramadhan Kayoko alikuwa ni mwamuzi wa kati kwenye mechi ya Ngao ya Jamii iliyowakutanisha Simba na Namungo, Agosti 30,2020 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid alitoa penalti moja kwa Simba baada ya nyota Bernard Morrison kuchezewa faulo ndani ya 18 na ilifungwa na John Bocco.

    Kwenye mchezo huo alitoa jumla ya kadi mbili za njano ambapo moja alimuonyesha Kocha Mkuu wa Simba wa zama hizo Sven Vandenbroeck na moja mchezaji wa Namungo Steve Duah ambaye alicheza faulo kwa Morrison.

    Pia kwenye mchezo huo alifanya kazi na Frank Komba  ambaye yupo kwenye orodha ya waamuzi wa leo.

    Waamuzi hawa waliwahi kufanya kazi pamoja pia kwenye dabi ya Kariakoo ilikuwa Julai 12 wakati Simba ikishinda mabao 4-1 ambapo mwamuzi wa kati alikuwa ni Kayoko aliyeibuka kuwa mwamuzi bora kwa msimu wa 2019/20 alishirikiana na Frank Komba.

    Kwa msimu huu wa 2021/22, Kayoko aliwahi kuwa mwamuzi wa kati kwenye dabi ambapo ilikuwa mchezo wa Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkapa,Septemba 25,2021 ambapo Yanga ilishinda bao 1-0.

    Kwenye mchezo huo walifanya kazi na Sasii na Komba na jumla ya kadi 8 za njano zilitolewa na Kayoko huku Taddeo Lwanga akionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

    Desemba 11,2020 wakati wababe hao wakitoshana nguvu bila kufungana mwamuzi wa kati alikuwa ni Sassi.

    Previous articleLIVERPOOL KAZINI LEO DHIDI YA NEWCASTLE
    Next articleYANGA YATAJA MABAO ITAKAYOIFUNGA SIMBA