LIVERPOOL KAZINI LEO DHIDI YA NEWCASTLE

KLABU ya Liverpool leo Aprili 30,2022 inatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Ni katika Uwanja wa St James Park mchezo huo unatarajiwa kupigwa ambapo kila timu inahitaji ushindi.

Liverpool ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 79 baada ya kucheza mechi 33 huku vinara wakiwa ni Manchester City wakiwa na pointi 80 nao wamecheza mechi 33.

Newcastle United wapo nafasi ya 9 na pointi zao ni 43 baada ya kucheza 34 ndani ya Ligi Kuu England.

Trent Alexander-Arnold ni moja ya mabeki wa kulia ambao wanapewa nafasi ya kuweza kuanza leo.