KIUNGO wa kikosi cha Manchester United, Paul Poga atasepa msimu ujao ndani ya kikosi hicho ambacho kinashiriki Ligi Kuu England.
Nyota huyo tayari ameshawaambia wachezaji wenzake kwamba msimu ujao hatakuwa ndani ya timu hiyo.
Pia inatajwa kwamba ameshajiondoa kwenye kundi la WhatsApp ambalo lilikuwa linawahusu wachezaji wa timu hiyo.
Kocha wa muda wa Manchester United, Ralf Rangnick alithibitisha kwamba nyota huyo atakuwa nje kwa muda baada ya kupata majeraha wakati timu hiyo iliponyooshwa mabao 4-0 dhidi ya Liverpool.
Mkataba wa Pogba mwenye miaka 29 unakaribia kufika ukingoni mwishoni mwa msimu huu.