SIMBA BADO HAWAIFIKIRII MECHI YAO DHIDI YA YANGA

UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa bado haufikirii mchezo wao dhidi ya Yanga kwa kuwa wametoka kucheza mechi kubwa ya hatua ya robo fainali dhidi ya Orlando Pirates.

Aprili 24 Uwanja wa Orlando, ubao ulisoma Orlando Pirates 1-0 Simba ikiwa ni mchezo wa hatua ya robo fainali ya pili na kufanya wawe wamefungana bao 1-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa Simba ilishinda bao 1-0.

Ilibidi mshindi apatikane kwa mikwaju ya penalti na hapo wawakilishi wa Tanzania kwenye mashidano ya kimataifa, Simba walifungwa penalti 4-3 ambazo waliweza kufunga.

Akizungumza na Saleh Jembe mara baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa bado wanafikiria mchezo wao uliopita.

“Tumerudi sasa ambacho tutaanza nacho ni kuangalia namna gani tuliweza kufanya kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya Orlando Pirates.

“Wenzetu wanafikiria kuhusu sisi ila sisi bado hatujaweza kuwafikiria kwa sasa mpaka muda kidogo uweze kupita hapo tutaweza kuwafikiria wapinzani wetu,”

Mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Yanga v Simba unatarajiwa kuchezwa Aprili 30, Uwanja wa Mkapa.