SIKU YA MALARIA DUNIANI IMEWAKUTANISHA MERIDIANBET NA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA AMANA

Katika kuadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa mwaka 2022, kampuni ya michezo ya kubashiri, Meridianbet, imeungana na watanzania na dunia kwa ujumla katika kuongeza nguvu kwenye mapambano makali dhidi ya ugonjwa wa Malaria. Ugonjwa wa Malaria unaripotiwa kuwa chanzo cha vifo vya watoto (hasa wenye umri chini ya miaka 5) na hivyo kwa sehemu kubwa, unachangia upungufu wa watu na kwa sehemu kubwa, nguvu kasi ya Taifa kwa vizazi vijavyo.

Meridianbet kwa kutambua madhara makubwa ya ugonjwa wa Malaria kwa wanajamii, imetumia fursa ya siku maalumu ya maadhimisho ya Malaria Duniani (Aprili 25, 2022) kuifikia jamii na hasa watoa huduma ya afya ambao ni watu muhimu katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa Malaria.

Kwa kutambua umuhimu wa watoa huduma wa Afya, Meridianbet iliitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ilikujumuika pamoja na watendaji wa hospitali hiyo katika jitihada adhimu za kuilinda na kuiokoa jamii kwenye janga la ugonjwa wa Malaria.

Hii imeendelea kuwa desturi na utamaduni wa Meridianbet kuifikia jamii kwa namna tofauti tofauti lengo likiwa ni kurudisha kwa jamii inayoizunguka. Ni dhahiri kuwa, Meridianbet pekee haiwezi kutatua changamoto au kuzifikia jamii zote zenye uhitaji na, kwakutambua hilo, Meridianbet wamekuwa wakishiriki na kuchangia kwenye matukio mbalimbali kadiri ya uwezo wao kwa wakati husika. Imani kubwa ya kampuni hii katika utaratibu huu ni kuisaidia jamii kwa kidogo kinachowezekana ili kwa pamoja, jamii zote ziwezekutekeleza majukumu yao ya kila siku zikiwa katika mazingira salama na wezeshi kiutelekezaji.

Mazingira ni kielelezo kimojawapo kinachohusiana moja kwa moja na kuenea kwa ugonjwa wa Malaria. Hili hudhihirika katika maeneo ambayo mazingira sio masafi na salama kwa jamii inayoishi au kutumia eneo hilo. Kwa kutambua umuhimu wa Mazingira, Meridianbet imechangia baadhi ya vifaa vya usafi wa mazingira kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ili kuiongezea nguvu hospitali hiyo kwenye muendelezo wa ufanyaji usafi kwenye mazingira yanayoizunguka. Pamoja na vifaa vya usafi, pia imechangia baadhi ya vifaa tiba ambavyo vitaongeza nguvu kwenye utoaji wa matibabu kwa jamii inayofika hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu mbalimbali.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo kutoka kwa wawikilishi wa Kampuni ya Meridianbet, Afisa Mahusiano wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana, Ndugu. Suphian Mndolwa, ameishukuru kampuni ya Meridianbet kwa kuitembelea hospitali hiyo na kuiongezea nguvu kwenye vifaa vya kiutendaji kazi hospitalini hapo. Aidha, ameongezea kuwa, bado hospitali hiyo inaendelea kuiasa jamii kujitokeza kwa wingi  kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wengi nchini wenye uhitaji wa damu ikiwa ni pamoja na kuiomba kampuni ya Meridianbet kuendelea kuwa karibu na jamii kwani, kwa kidogo wanachokirudisha kwa jamii, kinaokoa maisha ya wanajamii wengi zaidi.

Kwa upande wa Meridianbet, Afisa Maendeleo ya Jamii na Uhusiano, Ndugu. Amani Maeda aliushukuru uongozi mzima wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana kwa kupokea ombi la kampuni hiyo kufika hospitalini hapo na kuchangia kidogo walichonacho katika maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, 2022. Pia, Ndugu Maeda aliitumia nafasi hiyo kuwahimiza wadau na washirika wengine wa maendeleo kuwa na utamaduni wa kuzifikia jamii hasa zenye uhitaji kwa lengo la kuboresha mahusiano na kuwa karibu na jamii wanazozihudumia. Ameongeza kuwa, kama kampuni, watafanya jitihada za muhimu kwa kadiri itakavyowezekana ili wawezekushiriki kikamilifu katika zoezi la uchangiaji damu hospitalini hapo.

Meridianbet, Nyumba ya Mabingwa!! Bashiri Kistaarabu. HAIRUHUSIWI kwa wenye umri chini ya miaka 18.