WAWAKILISHI wa Tanzania, Simba kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho safari yao imefika mwisho leo nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti.
Ngoma ilikuwa nzito hasa kipindi cha kwanza, Simba walipiga mpira mkubwa kwa kujilinda huku viungo wakishindwa kutengeneza nafasi kwa mshambuliaji Chris Mugalu.
Kadi ya njano ya Mugalu ile ya pili iliwaondoa Simba mchezoni na kujichanganya kwa muda kisha wapinzani wao Orlando wakafunga bao la ushindi.
Idadi ilikuwa ni 1-1 na kuwafanya Simba waweze kwenda kuamua mchezo kwa mikwaju ya penalti hapo ndipo ugumu ulipokuwa.
Simba ilikosa penati mbili kupitia kwa Jonas Mkude na Henock Inonga huku Aishi Manula akiweza kuokoa penalti moja na ile ya mwisho iliyopigwa na kipa wa Orlando ilizama nyavuni.
Orlando wamefunga penalti 4-3 Simba kwenye mchezo wa leo ambao Simba walikuwa na kazi ya kulinda bao walilopata Uwanja wa Mkapa.