KLABU ya Manchester City imefikisha pointi 77 huku Liverpool ikiwa na pointi 76 zote zimecheza mechi 32 na City ni namba moja kwenye msimamo.
Ushindi wa mabao 3-0 Brighton and Hove Albion umetosha kuwarejesha tena kileleni.
Mabao Uwanja wa Etihad yalifungwa na Riyad Mahrez dk 53,Phil Foden dk 65 na Bernardo Silva dk 82.
City imewaacha Liverpool pointi moja na ina michezo sita mkononi ya kukamilisha ikiwa inatetea ubingwa wake.
Pep Guardiola bado yupo imara kwa kuwa alishuhudia mabao yote matatu yakifungwa kipindi cha pili.