TANZANIA YANUKIA KOMBE LA DUNIA

USHINDI wa mabao 4-0 walioupata Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 mbele ya Burundi umeiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kufuzu Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini India.

Ni mabao ya Clara Luvanda aliyetupia mabao mawili huku Neema Paul na Husna Ayoub wakitupia bao mojamoja iliamsha shangwe kwenye mchezo huo uliochezwa Aprili 16, nchini Burundi.

Tanzania sasa imebakiza michezo mitatu ambayo ni pamoja na ule wa marudiano dhidi ya Burundi,na inasubiri kumenyana na Zambia ama Cameroon kwenye mechi za mwisho.

Wakati wakicheza jana alikuwepo pia Naibu Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo,Pauline Gekul kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Urukundo kwenye mchezo huo wa raundi ya tatu.

Kocha Mkuu wa Tanzania, Bakari Shime amesema kuwa vijana walifanya kazi kwa juhudi na kufuata maelekezo jambo ambalo limewapa matokeo mazuri.