MWINA Kaduguda,Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba amesema kuwa watawafunga Orlando Pirates kwenye mchezo wao wa leo ili waweze kufanikisha lengo la kutinga hatua ya nusu fainali.
Leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Orlando unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
, Kaduguda amesema kuwa ana uhakika na ushindi kwa Simba kutokana na maandalizi pamoja na uwepo wa mashabiki wakutosha watakaojitokeza kuishangilia Simba.
“Wale Orlando Pirates walishawahi kuwa mabingwa wa 1995 walikuwa mabingwa wa Afrika sio timu ya kubeza na tusiwadharau ni watu wenye uzoefu lakini tunataka uzoefu wao uishie Uwanja wa Mkapa.
“Mashabiki wengi wakijitokeza na kushangilia kwa nguvu itawapa ari ya kupambana wachezaji wetu na inawezekana kabisa kushinda kwa kuwa tunahitaji ubingwa na kuacha habari za historia,” amesema Kaduguda.