POLISI Tanzania kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya Kwanza jana Aprili 16 walitoshana nguvu na Mbeya Kwanza.
Ni sare ya kufungana bao 1-1 iliweza kupatikana baada ya dk 90 kukamilika Uwanja wa Ushirika,Moshi.
Langoni alianza Metacha Mnata ambaye aliokota bao moja na kwa upande wa ushambuliaji ni Daruwesh Salioko na Kassim Haruna waliweza kupewa majukumu ya kusaka ushindi.
Watupiaji walikuwa ni Kasim Shaban dk 34 kwa Polisi Tanzania na Habib Kyombo dk 23 alifunga kwa upande wa Mbeya Kwanza.
Mabao yote yalipatikana kipindi cha kwanza na kile kipindi cha pili ngoma ilikuwa ngumu kwa timu zote mbili.
Sasa Polisi Tanzania inafikisha pointi 25 ikiwa nafasi ya 6 huku Mbeya Kwanza ikifikisha pointi 15 nafasi ya 16.