MANCHESTER UNITED NDANI YA TANO BORA

RALF Rangnick, Kocha Mkuu wa Manchester United ameshuhudia kikosi chake kikisepa na pointi tatu mazima mbele ya Norwich City.

Ni mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Old Trafford huku Cristiano Ronaldo akipachika mabao yote matatu na kusepa na mpira wake.

Ilikuwa dk ya 7,32 na 76 hayo yalitosha kuwapa furaha United ambayo bado haijawa kwenye kasi nzuri.

Kwa upande wa Norwich City ni mabao ya Kieran Dowell dk 45+1 na Teemu Pukki dk ya 52.

United inafikisha pointi 54 ikiwa nafasi ya 5 huku Norwich City ikiwa nafasi ya 20 na pointi 21.