RELLIATS Lusajo ni mtupiaji namba moja ndani ya kikosi cha Namungo FC na aliwahi kuwa namba moja ndani ya ligi alipofikisha jumla ya mabao 10.
Mara ya mwisho Lusajo kufunga ilikuwa ni Februari 25,2022 Uwanja wa Nyankumbu mbele ya Geita Gold ambapo alifunga bao lake la 10.
Mamo bado hayajajibu kwake muda huu kwenye upande wa kutupia mabao.
Kwenye mechi tatu mfululizo za ligi ilikuwa mbele ya Kagera Sugar,Azam FC na KMC alikwama kufunga wenye mechi hizo za ligi.
Kwa sasa Namungo FC inajiandaa kwa ajili ya mchezo wao wa ligi ujao dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa Jumatatu ya Aprili 18 Uwanja wa Ilulu.
Ni Fiston Mayele anayekipiga ndani ya Yanga kwa sasa ni namba moja kwa utupiaji akiwa ametupia mabao 11 na pasi 3 za mabao.