Home Sports NJOMBE MJI WAANZA NA KICHAPO 8 BORA

NJOMBE MJI WAANZA NA KICHAPO 8 BORA

WIDDEN Daphet, Kocha wa Njombe Mji amesema kuwa walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata jana katika mchezo wa hatua ya 8 bora.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa kundi A katika fainali za First League huko Mwanza.

Daphet amesema:”Tulishindwa kupata ushindi kwa kuwa hatukutumia nafasi ambazo tulizipata kwenye mchezo wetu.

“Lakini bado tuna nafasi katika mechi zijazo tutafanyia kazi makosa yetu ambayo tumeyafanya,”.

Alliance ilishinda mabao 2-0 Njombe Mji na Tunduru Korosho iliambulia kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers.

Kundi A vinara ni Rhino Rangers huku Alliance ikiwa nafasi ya pili zote zina pointi tatu na Tunduru Korosho ipo nafasi ya tatu huku Njombe Mji nafasi ya nne na hazina pointi.

Previous articleVIDEO:TAZAMA NAMNA ORLANDO PIRATES WALIVYOWASILI DAR
Next articleLUSAJO BADO HAJAFUNGA KITAMBO KWELI