ALLIANCE FC KUANZA NA NJOMBE MJI 8 BORA

WAKATI kesho Ijumaa michuano ya fainali ya Ligi Daraja la Kwanza hatua ya nane bora ikitarajia kuanza kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, Kocha Mkuu wa Alliance FC, Ibrahim Makeresa amesema kikosi chake kipo tayari kwa kazi.

Kocha huyo amesema kuwa kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi za hatua ya 8 bora.

 Makeresa amesema: “Tumejiandaa vyema vijana tayari wapo kambini toka tarehe 24 mwezi uliopita na tumetumia takribani wiki tatu na nusu hadi 4 hivi ili kuwaandaa wachezaji na kuhakikisha wapo vizuri kiufundi, kimbinu na kisaikolojia.

“Ijumaa sisi kama wenyeji tutafungua michuano hiyo kwa kucheza na wapinzani wetu Njombe Mji. Niwaombe wadau na mashabiki wote wa Alliance kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani tutakuwa nyumbani.”