VIDEO:SIMBA YATUPA DONGO KWA WATANI KIMTINDO,YAWAITA MASHABIKI

AHMED Ally, Meneja wa Kitengo cha Habari Mawasiliano ndani ya kikosi cha Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Orlando Pirates ambao ni hatua ya robo fainali na kuwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo huo kutimiza ile idadi ambayo wamepwa na CAF mashabiki 60,000.

Ameweka wazi kwamba wapo kamili wakiwa na uwanja wa mazoezi na wanachagua watumie ule wa nyasi bandia ama ule wenye nyasi za asili tofauti na wengine ambao wameweka kifusi.