UWANJA WA MKAPA: YANGA O-0 GEITA GOLD

DAKIKA 45 za burudani safi kabisa kutoka kwa timu zilizofanya maandalizi mazuri kutimiza kile ambacho wamepewa na benchi la ufundi.

Ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 0-0 Geita Gold ikiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.

Timu zote zinapambana kusaka ushindi huku umakini ukiwa ni tatizo kwenye kumalizia nafasi.

Zawadi Mauya amekuwa ni imara kwa Yanga kwa mipira ya mbali kuelekea langoni huku George Mpole akiwa kwenye uangalizi mkubwa wa Dickson Job.