SIMBA YAKIRI KUWA MCHEZO DHIDI YA POLISI TANZANIA UTAKUWA MGUMU

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mchezo wa kesho dhidi ya Polisi Tanzania utakuwa mgumu na ushindani mkubwa.

April 10,saa 10:00 jioni Simba itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania.

Leo wachezaji wa Simba wamefanya mazoezi ya mwisho ikiwa ni pamoja na Aishi Manula, Joash Onyango, Sadio Kanoute, Rally Bwalya kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika,Moshi ikiwa ni wa mzunguko wa pili.

Pablo amesema:”Utakuwa ni mchezo mgumu na tunajua hilo kwa kuwa wapinzani wetu nao wanahitaji pointi tatu nasi pia tupo tayari.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu hilo lipo wazi na kuhusu ubora wa uwanja hilo tutajua kesho namna itakavyokuwa na vile ambavyo tutafanya,”.

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya pili na pointi 40 baada ya kucheza mechi 18 inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya 9 na pointi 23.