Home Sports SIMBA KUWA TIMU YA KWANZA KUTUMIA VAR BONGO

SIMBA KUWA TIMU YA KWANZA KUTUMIA VAR BONGO

WAWAKILISHI wa Tanzania Simba kwenye mashindano ya kimataifa wanakwenda kuandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutumia mfumo wa msaada wa VAR kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Tokea VAR ianze kutumika katika mchezo wa soka duniani, haijawahi kutumika kwenye Uwanja wowote nchini na Simba iliyofikia hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika inakwenda kuwa ya kwanza.

Mechi nyingine za hatua hiyo pia zitatumia mfumo huo.

Maanayake ni kwama mchezo wao wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa Aprili 17, 2022 Uwanja wa Benjamin Mkapa, waamuzi watatumia msaada wa video (Video Assistant Referee-VAR).

Orodha ya waamuzi wa mchezo huo imeshajulikana sambamba na wale watakao ongoza VAR.

Hawa hapa waamuzi:-

Referee: Haythem Guirat (Tunisia)
Assistant Referee 1: Khalil Hassani (Tunisia)
Assistant Referee 2: Samuel Pwadutakam (Nigeria)
Fourth Official: Sadom Selmi (Tunisia)
Video Assistant Referee: Ahmed Elghandour (Misri)
Assistant VAR: Youssef Wahid Youssef Misri.

Caf wameshatoa taarifa kuhusiana na uwepo wa matumizi ya VAR kwenye mchezo huo jijini Dar es Salaam.

Previous articleMBEYA KWANZA SIYO YA KWANZA KWA SASA
Next articleBREAKING:UWANJA WA MKAPA MASHABIKI 60,000 SIMBA V ORLANDO PIRATES