PAUL Merson kiungo wa zamani wa Arsenal amesema kuwa wapinzani wake wa zamani Tottenham Hotspur wana nafasi ya kumaliza ndani ya Top 4 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Nyota huyo ameweka wazi kuwa ikiwa mshambuliaji wa timu hiyo Harry Kane akiumia mambo yatakuwa ni magumu zaidi kwao.
Ikumbukwe kwamba hata Arsenal inawania nafasi ya kumaliza ndani ya Top 4 ilinyooshwa mabao 3-0 dhidi ya Crystal Palace jambo ambalo anaamini kwamba ni udhaifu mkubwa kwa Arsenal.
“Kipigo cha Jumatatu kilikuwa kinaogopesha. Spurs ndio timu ambayo ina nafasi zaidi ya kuweza kutiga ndani ya Top 4. Kama Harry Kane akicheza kama anavyocheza sasa, sidhani kama kuna timu nyingi zitawafunga.
“Lakini ukimuondoa Kane kwenye timu Top 4 haiwezi kutokea kwao alipokosekana shidi ya Burnley walifungwa ile inaonekana kuwa ni timu ya mchezaji mmoja,”.