TATIZO LA MAPIGO HURU LINAITESA SIMBA,JASHO ILIMWAGIKA KIMATAIFA

    USIKU wa deni haukawii kukucha walisema wahenga na ilikuwa hivyo Uwanja wa Mkapa kwa wawakilishi wa Tanzania kimataifa kuweza kutimiza jambo lao.

    Ilikuwa ni lazima ishinde ili itinge hatua ya robo fainali kama haari ingekuwa nyingine,safari ingewakuta Simba waliokuwa wakisaka ushindi mbele ya USGN.

    Jasho na machozi ya furaha yalimwagika kwa Mkapa baada ya ubao kusoma Simba 4-0 USGN,makala haya yanakuletea msako ulivyokuwa na sasa ikiwa ni hesabu za kwenye hatua ya robo fainali ambapo itacheza na Orlando Pirates ya Afrika Kusini:-

    Pablo

    Kocha Mkuu wa Simba kete alizopanga kuimaliza USGN ziliweza kujibu ikiwa ni pamoja na Chris Mugalu ambaye alikuwa ameyeyusha dk 41 kwenye mechi za hatua ya makundi za awali ilikuwa mbele ya ASEC Mimosas na RS Berkane na zote alianzia benchi lakini juzi alianza kikosi cha kwanza.

    Tatizo la mipira iliyokufa lipo palepale

    Mapigo huru bado ni tatizo kwa Simba, kwenye mchezo dhidi ya USGN juzi ni kona 12 walipiga na katika hizo hakuna hata moja iliyoweza kuwa na hatari langoni mwa USGN.

    Mbinu zote za kona ndefu na zile fupi ziligonga mwamba, Rally Bwalya yeye alikuwa anapiga kona ndefu alifanya hivyo dk ya 15,28,29 na 58.

    Bernard Morrison yeye alipiga kona dk ya 4,5,20,21,25,29,30 na 67 katika hizo zipo ambazo alipiga mapigo mafupi ila hazikuleta hatari kwa USGN.

    Walitembeza pini za maana

    Sadio Kanoute muache tu akiwa uwanjani ni mwendo wa pini kimyakimya na alikuwa na kazi hiyo alifanya hivyo dk 44 akaonyoshwa kadi ya njano.

    Joash Onyango aliona isiwe tabu alikwenda mazima na mshamuliaji matata wa USGN Victorean Adebayo ilikuwa dk ya 40 kwa kumzuia asimfuate Aishi Manula baada ya kuzidiwa maarifa na alionyeshwa kadi ya njano.

    Dakika 45 za mwanzo zilikuwa chungu

    Zilikuwa ni dakika chungu kwa mashabiki wa Simba na wachezaji kwa kuwa kila nafasi waliyokuwa wakiamini inazamishwa nyavuni inakwenda nje ya lango.

    Ilikuwa hivyo dk ya kwanza kupitia kwa Jonas Mkude,Kanoute dk ya 6 na 38, Pape Sakho dk ya 32 na 45, Bwalya dk ya 45 Onyango dk ya 15.

    Mabeki walijenga ukuta

    Onyango alikuwa na kazi kubwa eneo la ulinzi na safu kwa ushirikiano mkubwa na Henock inonga,Shomary Kapome na Mohamed Hussein ambao wote walikuwa wanapanda na kushuka.

    Kapombe mbali na kupewa jukumu la mipira ya kurusha ambapo alifanya hivyo dk ya 3,7,24 na 38 pia aliweza kutibua mipango ya USGN ilikuwa dk ya 4,34.

    Zimbwe yeye alikwama kuyeyusha dk 90 aliumia dk ya 0 lakini aliweza kutibua mipango dk ya 14 na 45 na alipiga faulo dk ya 59.

     Inonga alikuwa ni beki wa kupanda na kushuka, aliweza kutibua mipango dk 9,13 alicheza kwa utulivu mkuwa.

    Wazee wa kukera

    Bernard Morrison alikuwa mzee wa kukera na alikuwa anapata utulivu mkubwa kutokana na uwepo wa kiungo Jonas Mkude aliyekuwa akisambaza pasi za upendo eneo la kati.

    Morrisson alisababisha kona 4 na alipiga faulo moja iliyolenga lango ilikuwa dk ya 55, alitoa pasi mbili za mabao kwa Kanoute na Mugalu alitumia dk 79 nafasi yake ilichukuliwa na Taddeo Lwanga.

    Sakho licha ya kushindwa kufunga alikuwa anakera jambo lililofanya awe  miongoni mwa wachezaji waliochezew faulo ilikuwa dk ya 12,14 na 59 na aliotea dk ya 18 alitumia dk 63 nafasi yake ilichukuliwa na Kiu Dennis.

    Walibadili ubao

    Sadio Kanoute dk 62,Chris Mugalu alitupia mabao mawili ilikuwa dk ya 68,79 na kipa wa USGN Saidu Hamisu alijifunga dk 83 katika harakati za kuokoa mpira.

    Manula

    Aishi Manula aliweka lango salama aliweza kuokoa michomo dk ya 9,34,35,44,46 na 70.

    Adebayo aliwapa tabu

    Mshambuliaji wa USGN, Victorean Adebayo aliwapa tabu mabeki wa Simba kutokana na kuweza kufanya majaribio mawili ambayo hayakulenga lango akiwa nje ya 18 ilikuwa dk ya 67 na 74 dk ya 44 alipiga shuti lililolenga lango na kuishia mikononi mwa Manula.

    @Dizo_Click.

     

    Previous articleKAMPUNI YA MERIDIANBET TANZANIA YATOAMKONO WA POLE
    Next articleKUMALIZA TOP 4 KWA TOTTENHAM KUNAMTEGEMEA KANE