HESABU za Simba baada ya kumaliza mchezo wao jana Aprili 7 mbele ya Coastal Union na ubao wa Uwanja wa Mkwakwani kusoma Coastal Union 1-2 Simba ni dhidi ya Polisi Tanzania.
Simba ni mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya pili na pointi 40 inakwenda kukutana na Polisi Tanzania Aprili 10,2022.
Polisi Tanzania kwenye msimamo ipo nafasi ya 9 na ina pointi 23 baada ya kucheza mechi 18 sawa na zile ambazo Simba imecheza.
Pablo Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanahitaji ushindi kwenye mechi ambazo watacheza ndani ya ligi.
“Tunajua ushindani ni mkubwa na tutafanya kazi kusaka ushindi kwenye mechi ambazo tutacheza kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi,”.
Katika mchezo mbele ya Coastal Union ni Victor Ackpan aliweza kumtungua Aishi Manula na Bernard Morrison alipachika bao la kuongoza kwa Simba na lile la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere kwa pasi ya Chris Mugalu.
Kagere anakuwa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Simba akiwa ametupia mabao 7 na ametoa pasi moja ya bao.