ISHU YA KUONGEZWA DAKIKA 100 KWENYE MECHI IPO HIVI

BAADA ya hivi karibuni taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya Fifa kuangalia uwezekano wa kuongeza dakika za mchezo wa mpira wa miguu kutoka 90 hadi 100 kabla ya mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia la nchini Qatar, FIFA imeibuka na kukanusha taarifa hizo.

Taarifa kutoka fifa imesema:“Kufuatia taarifa za uzushi zilizosambaa leo, FIFA inapenda kuliweka sawa swala hili kwamba hakutakuwa na mabadiliko yoyote yale kuhusiana na muda wa kucheza mpira wa miguu uwanjani katika mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia la nchini Qatar 2022, au katika mashindano mengine yeyote yale.”

Taarifa hizo zimeibuka baada ya Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Masuala ya Michezo CIES kutoa takwimu kwamba zaidi ya dakika 30 zinapotea kwenye kila mchezo wa kawaida wa dakika 90 kutokana na kupoteza muda (Time-wasting) na kurusha mipira inayokuwa imetoka (Throw-ins)