LEO NI LEO ITAFAHAMIKA UWANJA WA AZAM COMPLEX

ZOTE mbili ni za moto kwa sasa kwa kuwa zimetoka kushinda mechi zao zilizopita na kujiwekea pointi tatu kibindoni.

Ni Azam FC iliyotoka kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Ilulu na Yanga iliyotoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya KMC

Leo wana kazi ya kusaka pointi tatu muhimu kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku itafahamika nani ni nani.

Moto upo hapa

Moto upo kwenye safu ya ushambuliaji ambapo rekodi znaonyesha kwamba yule aliyekuwa wa mwisho kuifunga Yanga na ikapoteza pointi mazima kwenye ligi amerejea kwenye ubora.

Ni Prince Dube ambaye aliweza kufanya hivyo ilikuwa ni Aprili 25,2021 Uwanja wa Mkapa na ubao ulisoma Yanga 0-1 Azam FC.

Dube alifunga bao lake la kwanza kwenye ligi Uwanja wa Namungo hivyo moto wake unaweza kuendelea leo ama maji yakapoa.

Fiston Mayele

Mchezaji mwenye kasi kubwa na jicho la kufunga akiwa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga na ametupia mabao 10 na pasi tatu za mabao.

Amehusika katika mabao 13 kati ya 31 ambayo yamefungwa na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 48 na ni mechi 18 kacheza.

Watawaachaje mashabiki?

Timu zote mbili zinahitaji kuwaacha mashabiki kwa mtindo wao ambapo Azam FC inahitaji kuwapa tulizo baada ya ule mchezo wa kwanza kunyooshwa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.

Kwa upande wa Yanga wao wanahitaji kuendelea pale ambapo waliishia ili wasitibue rekodi yao ya kushinda mechi zao.

Heshima v ubingwa

Ikiwa Azam FC itashinda kesho itakuwa ni timu ya kwanza kuifunga Yanga ndani ya ligi ambayo imecheza mechi 18 bila kufungwa.

Yanga hesabu zao ni kushinda ili kufungua njia ya kufikia ulipo ubingwa ambao kwa sasa upo mikononi mwa Simba iliyo nafasi ya pili.

Yanga namba moja

Yanga inaonekana kuwa bora kila idara kwa msimu huu tofauti na Azam FC,ukianza na ile safu ya ushamuliaji Yanga imetupia mabao 31 huku Azam FC ikiwa imetupia mabao 22 tofauti ya mabao 9.

Ukigusa safu ya ulinzi ni mabao 4 ambayo Yanga imefungwa na Azam FC imefungwa jumla ya maao 16 tofauti ya mabao 12.

Ukigusa pointi Azam kibindoni wana pointi 28 nafasi ya tatu na Yanga ni nafasi ya kwanza point 48 tofauti ya pointi 20.

Abdi Hamid Moallin, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa kwake binafsi Yanga ni timu bora nchini kwa sasa.

“Yanga ndiyo klabu bora nchini unapaswa kucheza na walio ora li uweze kuwa bora mchezo wetu dhidi ya Yanga tunataka kuuchukulia tofauti kama ule wa Namungo.

 “Alama 20 mbele yetu nab ado hawajapoteza hilo ni kubwa hivyo kwetu ni fursa kuweza kucheza nao na tunajiaandaa kwa ajili ya mchezo huo,”

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anatambua mechi ambazo zinakuja ni ngumu ila anahitaji ushindi.

“Ninatambua kwama kuna mechi ngumu zinakuja kwani baada ya KMC inafuata Azam FC huu ni mchezo ambao unahitaji umakini mkubwa na kikubwa ni ushindi.

“Haitakuwa kazi rahisi kwetu nimewaambia wachezaji kuwa kazi ni moja kutafuta ushindi na inawezekana kwa kuwa mimi ninapenda kuona tukicheza na kushinda kwa vitendo,” alisema.

@Dizo_Click