KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam Abdi Hamid Moallin amekubali ubora wa kikosi cha Yanga na kuweka wazi kwamba anaandaa mbinu ili kuwakabili vinara wa Ligi Kuu Bara.
Moallin amesema kuwa anatambua kwamba wameachwa kwa pointi nyingi na wapinzani hao ambao wanaongoza ligi kwa wakati huu.
“Ninatambua kwamba Yanga ni timu imara na inaongoza ligi kwa sasa hivyo lazima tucheze nao kwa tahadhari ili kuweza kusaka pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo.
“Tumetoka kushinda mbele ya Namungo hilo tunajua lakini tutakuwa tofauti kwenye mchezo wetu mbele ya Azam FC maandalizi yapo sawa,”.
Leo saa 2:05 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex. na kikosi hicho jana kimefanya mazoezi a mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo.
Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye mazoezi ni pamja na Prince Dube, Ibrahim Ajibu,Bruce Kangwa.