SIMBA YAPANIA KUWAFUNGA RS BERKANE KWA MKAPA

BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba SC, amesema wapinzani wao RS Berkane kwenye mchezo unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili hii, hawatatoka salama. Simba inatarajiwa kumenyana na RS Berkane ya Morocco kwenye mchezo wa nne wa Kundi D, wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita ugenini kwa kufungwa mabao 2-0. Barbara amebainisha kuwa, kwa maandalizi…

Read More

MUACHENI AIR MANULA AWE AIR KWENYE KAZI

AISHI Manula, ‘Air Manula’ kipa namba moja wa Simba ni Air Manula kwelikweli kama anavyopenda kuitwa kwa kuwa amewafunika makipa wote kwa upande wa kucheza mechi nyingi na kuwa namba moja kufungwa mechi chache. Pongezi kubwa kwa ukuta wa Simba unaongozwa na Joash Onyango pamoja na Henock Inonga ambao umeweza kumshuhudia kipa wao akiokota mabao…

Read More

MTAMBO WA MABAO YANGA UPO KAMILI GADO

FISTON Mayele, nyota wa kikosi cha Yanga yupo kamili gado kwa ajili ya mwendelezo wa mechi za ushindani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho. Mayele alipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba. Kwenye mchezo huo Mayele alikwama kuyeyusha dakika 90 na aliweza…

Read More

SIMBA UGENINI WANAPATA MATESO KWELIKWELI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kwa msimu wa 2021/22 wamekuwa wakipata mateso makubwa ugenini katika msako wa pointi tatu kwa kuwa mambo yamekuwa ni magumu kwao. Kwa mzunguko wa kwanza katika mechi 15 ambazo wamecheza na kuweka kibindoni pointi 31 ni mechi 7 walicheza ugenini na kushinda 3 huku wakiambulia sare 2 na…

Read More

MAYELE ATAJWA KUINGIA RADA ZA KAIZER CHIEFS

IMEELEZWA kuwa Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inataka kumsajili mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele (27) ili akawe mbadala wa mshambuliaji wao, Sebia Samir Nurković (29) ambaye huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu. Mayele amekuwa na kiwango bora ndani ya kikosi cha Yanga ambapo mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 10 na…

Read More

BILIONEA WA UINGEREZA ATAKA KUINUNUA CHELSEA

BILIONEA kutoka nchini Uingereza na shabiki mkubwa wa Chelsea, Nick Candy amethibitisha kuwa na nia ya kutaka kuinunua Klabu ya Chelsea ambayo imewekwa sokoni na mmiliki wake, bilionea kutoka Urusi, Roman Abramovic. Bilionea Candy ameweka mezani ofa ya kiasi cha paundi bilioni 2.5 pamoja na nyongeza ya paundi bilioni 1.5 kwa ajili ya matengenezo ya…

Read More

VIDEO:UJUMBE WA BARBARA HUU HAPA

BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amebainisha kwamba ni kawaida kwa Simba kuweza kuadhimisha kipekee Siku ya Wanawake Duniani ambapo Machi 8,2022 waliweza kutembelea Gereza la Wanawake pia waliwezza kutoa msaada ambapo aliweza kutoa ujumbe kwa mashabiki wa Simba pamoja na Watanzania kiujumla.

Read More

AZAM FC WAPITIA KIKOMBE CHA MATESO DK 270

KILE kikombe cha mateso ambacho wachezaji wa Simba walikuwa wanakipitia kwa muda wa dakika 270 bila kufunga kwenye mechi tatu mfululizo sasa kimebebwa jumlajumla na Azam FC. Ikumbukwe kwamba Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco ilipitia msoto huo Januari 17,2022 iliponyooshwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kisha kikombe kikaendelea mpaka Januari 22,2022 walipotoshana…

Read More

PRISON WATENGA MECHI ZA USHINDI

KOCHA Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Kazumba ameweka wazi kwamba mechi nne zijazo mbele zitawafanya warudi kwenye ubora wao. Timu hiyo kwa sasa inatumia Uwanja wa Sokoine kama ilivyokuwa ikifanya zamani baada ya kuhamia Uwanja wa Nelson Mandela, Songea wakati walipokuwa kwenye maboresho ya kambi yao. Prisons ipo kwenye mwendo wa kusuasa msimu wa 2021/22…

Read More

MZUNGUKO WA PILI UWE NA UTOFAUTI ZAIDI

MZUNGUKO wa pili unazidi kumeguka taratibu ni kama vile ambavyo mzunguko wa kwanza ulianza kwa msimu wa 2021/22 hasa kwa timu kusaka ushindi. Ipo wazi kwamba mzunguko wa maamuzi huwa huu wa pili kwa kuwa kile ambacho unakivuna wakati huu utapata majibu yake mwisho wa msimu. Zile ambazo zipo nafasi za kushuka daraja wakati mwingine…

Read More

SIMBA:RS BERKANE WAMEKUJA WAKATI MBAYA,MUGALU AREJEA

AHMED Ally Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa wapinzani wao wamewakuta wakiwa kamili kutokana na wachezaji wote kuwa tayari kwa mchezo huo. Simba itamenyana na RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 13. Ally amesema:”Taarifa ya awali kuhusu majeruhi ni kuwa Hassan Dilunga…

Read More

MAYELE HATARI YAKE KILA DAKIKA 100

KINARA wa utupiaji wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga, Fiston Mayele ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 100 awapo uwanjani kwenye kutupia pamoja na kutengeneza nafasi za mabao. Ndani ya Ligi Kuu Bara ameyeyusha dakika 1,301 akiwa amefunga mabao 10 na ni mabao matano ametupia Uwanja wa Mkapa huku mabao…

Read More

LAUTARO AVUNJA MWIKO WA LIVERPOOL

LAUTARO Martinez nyota wa kikosi cha Inter Milan alivunja rekodi ya Klabu ya Liverpool kutopoteza mchezo wa ushindani katika mechi zake za Uwanja wa Anfield baada ya kuwatungua bao dakika ya 61. Ni katika mchezo wa UEFA Champions League uliochezwa Uwanja wa Anfield ambao ulikuwa ni wa raundi ya 16 ukiwa ni mchezo wa pili….

Read More