MORRISON:TUTASHINDA MCHEZO WETU

KIUNGO wa Simba, mchetuaji Bernard Morrison amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya USGN na watapambana ili kupata matokeo chanya.

Simba inakibarua cha mwisho mkononi cha kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ikiwa na pointi zake kibindoni 7 baada ya kucheza mechi tano.

Kufungwa 3-0 mbele ya ASEC Mimosas, Machi 20,2022 kuliyeyusha matumaini ya Simba kutangulia katika hatua ya robo fainali hivyo wana kazi ya kufanya Uwanja wa Mkapa.

“Tulipoteza mchezo lakini hatujapoteza matumaini hivyo mchezo wetu ujao tunaamini kwamba tutafanya vizuri na tutapata matokeo, kikubwa ni mashabiki kuweza kujitokeza.

“Ikiwa tunacheza mchezo wa maamuzi hakuna ambaye anaweza kukubali kuona tunafungwa,tunajiamini na tutakuwa nyumbani hapo kazi itafanyika,”

Mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali unatarajiwa kuchezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.

Ili Simba iweze kufuzu hatua ya robo fainali inahitaji ushindi katika mchezo huo.