BARCELONA YAISAKA SAINI YA LEWANDOWSKI

IMEELEZWA kuwa Klabu ya Barcelona inaisaka saini ya staa Robert Lewandowski ambaye ni mshambuliaji ili kuweza kuwa naye kwa msimu ujao ndani ya kikosi hicho.

Lewa ni moja ya mastaa ambao wana ushkaji mkubwa na kucheka na nyavu alikuwa anatajwa pia kuwindwa na Manchester United.

Staa huyo wa Klabu ya Bayern Munich mkataba wake umesalia mwaka mmoja na mabosi wake wanaonekana kwamba hawana mpango wa kumpa mkataba mpya.

Ikiwa Barcelona wataongeza nguvu wanaweza kumnunua kwa wakati ujao ama wakavuta subira mpaka mkataba wake utakapoisha ili aweze kujiunga bure na timu hiyo.

Tayari Barcelona ipo na nyota mpya Aubameyang ambaye anafanya vizuri kwenye mechi za hivi karibuni.