SportsWINGA JESUS MOLOKO ANAREJEA MDOGOMDOGO Saleh4 years ago01 mins WINGA wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi emeanza kurejea mdogomdogo katika ubora wake. Ni Jesus Moloko ambaye alikuwa chaguo la kwanza la Nabi kabla hajapata maumivu hivi karibuni. Mchezo wake wa mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa ni dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Ilikuwa ni Februari 23,2022 na ubao ulisoma Yanga 0-0 Mbeya City ila kwa sasa taarifa zimeeleza kuwa anaendelea vizuri. Kwenye msimamo Yanga ni namba moja ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 18 na haijapoteza mchezo hata mmoja ndani ya ligi. Post navigation Previous: KISA MAYELE SIMBA WAONYWANext: MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO
Soccer Football - International Friendly - Spain v Brazil - Santiago Bernabeu, Madrid, Spain - March 26, 2024 Spain's Rodri scores their third goal from the penalty spot REUTERS/Violeta Santos Moura Je Fainali ya Kombe la Dunia 2026 Itakuwa Brazil vs Hispania? Saleh2 days ago 0