WACHEZAJI TUKUMBUKE KUWALINDA WACHEZAJI

    WAKATI mwingine sasa kuweza kuangalia yale makosa ambayo yalifanyika mzunguko wa kwanza kabla ya kuweza kuboresha mambo zaidi mzunguko wa pili.

    Kwa mzunguko wa kwanza tumeshuhudia namna ambavyo kila timu ilikuwa inapambana kusaka ushindi na kupata kile ambacho kilikuwa kinapatikana baada ya dakika 90.

    Ilikuwa ni muda bora kwa wachezaji kusaka ushindi kwenye mechi ambazo waliweza kucheza na wale ambao walikuwa benchi nina amini kwamba kuna kitu walijifunza.

    Tulishuhudia ile migongano ya hapa na pale na tuliweza kuweka wazi kwamba wakati huu sio muda wa kuendelea kuumizana tena na badala yake ni muhimu kila mmoja akawa mlinzi wa mwingine.

    Hakuna namna jambo la msingi kwa sasa ni kuona kwamba hakuna ambaye anampotezea muda mwenzake kuwa nje ya uwanja kwa kumuumiza hilo halipo sawa.

    Kila mchezaji mzunguko wa pili ni lazima awe mlinzi wa mchezaji mwenzake haya ni maisha na hakuna haja ya kukomoana kwenye mechi ambazo mtakuwa mnacheza.

    Jambo la msingi ni kuona kwamba kwa sasa ni kuona kwamba kila kinachopangwa kinapatikana na kama ilishindikana mzunguko wa pili basi wakati huu ni kuweza kuona inawezekanaje kupatikana.

    Haitakuwa rahisi kuweza kupatikana kwa haya yote kama hakutakuwa na maandalizi sahihi kwenye mechi ambazo timu itakuwa inacheza na hilo lipo wazi.

    Tukirudi kwenye jamvi la leo ninapenda kuweka wazi kwamba zipo timu ambazo hazikuwa na mwendo mzuri kwa mzunguko wa kwanza na sasa ni mzunguko wa pili.

    Ikiwa ziliweza kuona namna ambavyo ilikuwa ngumu kwao kupata matokeo basi muda wa kuweza kuleta mabadiliko kwenye mechi za mzunguko wa pili ni sasa.

    Kila mmoja na afanye kazi kwa juhudi katika kutimiza majukumu yake na hili ni muhimu kwa kuwa hakuna ambaye anaamini kwamba anaweza kupata ushindi ikiwa hataweza kujiweka vizuri.

    Wachezaji jukumu lenu kubwa kushirikiana uwanjani wakati wa kusaka matokeo na sio suala la kumuachia mchezaji mmoja hilo sio sawa.

    Ikiwa mbinu za mwalimu wakati mwingine zinakataa hapo akili kubwa kwenye miguu yenu na ubongo ni muhimu kuweza kuamua matokeo.

    Jambo la msingi ambalo mashabiki wanahitaji ni matokeo na huwa hayabadiliki wakati wote huwa yanakuwa ni sare,kushinda ama kushindwa yote haya yanaihusu timu.

    Kwa suala la kushuka hilo haliepukiki hivyo kwa timu ambazo zilikuwa kwenye mwendo wa kusuasua mzunguko wa kwanza ni wakati wa kuweza kushtuka sasa na kupambana zaidi ya wakati uliopita.

    Yale malengo ambayo yalikuwa yamewekwa mzunguko wa kwanza basi lazima yatazamwe kisha kwa sasa kila mmoja aweze kuanza kutimiza majukumu tofauti na wakati ule.

    Kila kitu kinawezekana jambo la msingi ni juhudi na kufanya kazi kwa kushirikiana huku kila mchezaji akiwa ni mlinzi wa mchezaji mwenzake.

    Previous articleRATIBA YA MECHI ZILIZO KATIKA KALENDA YA FIFA ZITAPIGWA KWA MKAPA
    Next articleAKILI ZA SIMBA SASA NI KWENYE LIGI