SERENGETI GIRLS WAREJEA BONGO NA USHINDI

TIMU ya Taifa ya Wasichana U 17,’Serengeti Girls ‘ usiku wa kuamkia leo wamewasili salama Dar wakitokea Botswana.

Serengeti Girls ilikuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Botswana mchezo uliochezwa Machi 20,2022.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Obeid Itan Chilume wa Botswana ulisoma Botswana 0-4 Tanzania na kufanya Tanzania ishinde kwa jumla ya mabao 11-0.

Ushindi huo unaifanya Tanzania kuweza kutinga raundi ya 3 katika Kombe la Dunia na inatarajiwa kucheza na timu ya Taifa ya Burundi.

Walipokelewa na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) pamoja na Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.