ILITOKEA hali ambayo ilisababisha mchezo kati ya Ajax v Feyenoord kuchelewa kuanza kwa muda kutokana na tukio la moto kutokea upande mmoja katibu na lango la timu moja.
Ajax ilipoteza katika mchezo huo uliochezwa Jumapili katika Uwanja wa Johan Cruyff Arena.
Baada ya mchezo huo kuanza na kuchezwa ubao ulisoma Ajax 3-2 Feyenoord na ni mabao ya Sebastien Haller dk 24,Dusan Tadic dk ya 78 na Antony dk 90+4 ambaye pia alionyeshwa kadi nyekundu.
Yale ya Feyenoord yalifungwa na Luis Sinisterra dk ya 8 na Guus Til dk 28 ndani ya Eredivisie ambayo ni ligi ya Netherlands.
Hali hiyo ilitokea inasadikika kuwa ilisababishwa na mashabiki timu iliyokuwa nyumbani katika mchezo huo na hakuna ambaye ameumia.