SIMBA YAPOTEZA KIMATAIFA BAO 3-0 YACHAPWA

UGENINI Simba imepoteza kwa kufungwa mabao 3-0 huku mabao yakipachikwa na Aubin Kramo Kouame dk 16,Stephane Aziz dk 23 na Karim Konate dk 57.

Licha ya Air Manula kuokoa penalti mbili bado kazi ilikuwa ngumu kwa washambuliaji kuweza kucheka na nyavu.

Katika kundi D sasa pointi inashushwa kutoka nafasi ya kwanza mpaka nafasi ya tatu ikibaki na pointi 7.

ASEC Mimosas inakuwa ni namba moja ina pointi 9 baada ya kucheza mechi 5 huku Simba ikiwa na pointi hizo 7 nafasi ya 3.

RS Berkane nafasi ya pili ina pointi 7 na imecheza mechi tano na ni USGN ipo nafasi 4 ikiwa na pointi 5.

Kundi hili sasa kuweza kutinga hatua ya nusu fainali ni mechi moja itaamua nani atakuwa nani huku ASEC Mimosas ikiwa ipo katika nafasi ya kuweza kutinga hatua ya robo fainali.