KISA KUSHANGILIA LAMPARD AVUNJIKA,ALLAN ALIMWA NYEKUNDU

FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Everton amesema kuwa amevunjika mkono wakati wa kushangilia bao la ushindi timu yake ilipokuwa ikicheza dhidi ya Newcastle.

Mchezo huo wa Ligi Kuu England ulichezwa Machi 17 na ubao wa Uwanja wa Goodison Park ulisoma Everton 1-0 Newcastle United.

Bao la ushindi lilipachikwa na Alex Iwobi dakika ya 90+9 ikiwa ni mchezo wa tatu wa timu hiyo kushinda ndani ya ligi msimu huu tangu iliposhinda Septemba baada ya hapo Lampard aliweza kueleza hali ya mkono wake.

“Sijui ilikuaje ila nilifanya katika kushangilia bao nadhani kuna muunganiko wa jambo fulani ila niligundua baadaye nilipojaribu kuchezesha mkono wangu ila ninachukua hayo kwa ajili ya pointi tatu,”.

Kwenye mchezo huo mchezaji wa Everton Allan alionyeshwa kadi nyekundu ilikuwa dk ya 83 atakosekana kwenye mechi tatu zijazo.

Kwa upande wa Alan Shearer wanapenda kumuita Mr Newcastale amesema kuwa alishangazwa na kadi hiyo nyekundu.

Everton ipo nafasi ya 17 na pointi 25 inapambana kubaki ndani ya ligi huku Newcastle ikiwa nafasi ya 14.