RALF Rangnick, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa walishindwa kutumia vizuri nafasi ambazo walizipata kipindi cha kwanza jambo ambalo liliwafanya wapoteze mchezo wao.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Old Trafford ulisoma Manchester United 0-1 Atletico Madrid.
Matokeo hayo yanaiondoa mazima United katika UEFA Champions League kwa jumla ya mabao 1-2 ambayo wameshinda Atletico.
Madrid Mtupiaji wa bao pekee la ushindi kwa Atletico Madrid alikuwa ni Renan Lodi dk 41.
Rangnick amesema:”Tulikuwa na kipindi cha kwanza kizuri lakini tulishindwa kutumia nafasi ambazo tulizipata ikawa bahati mbaya kwetu tukapoteza mchezo,”.
Hayo ni majanga mengine kwa United kuweza kushindwa kutinga hatua inayofuata ambapo awali ilikuwa inapewa nafasi ya kuweza kufanya vizuri.